5.7 C
New York

Ndege iliyopotea kuanza kutafutwa Desemba 30

Published:

KUALA LUMPUR, Malaysia

IKIWA ni miaka 14 imepita tangu ilipopotea, Serikali ya Malaysia itaanza tena operesheni ya kuisaka ndege yake aina ya Boeing 777. Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa katika taarifa ya leo ya Wizara ya Usafirishaji, operesheni hiyo itaanza Desemba 30, mwaka huu.

Ndege hiyo, Boeing 777, ilipotea Machi 8, 2014, ikiwa na abiria 239, wengi wao wakiwa ni raia wa China, ikiwa inaelekea Beijing. Licha ya jitihada kubwa za kuitafuta, haikuweza kuonekana, huku tukio hilo likitajwa kuwa ni kubwa zaidi katika historia ya usafiri wa anga duniani.

“Operesheni ya msako wa baharini itafanyika kwa siku 55,” ilieleza taarifa ya jana ya Wizara ya Usafirishaji.
Operesheni ya awali iliongozwa na Australia lakini ilisitishwa baada ya makubaliano ya nchi tatu, zikiwamo China na Malaysia.

Aidha, uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa Kusini mwa Bahari ya Hindi ulishindwa kuendelea kutokana na hali mbaya ya hewa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img