MADRID, Hispania
MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko zimeathiri safari za ndege nchini Hispania.
Kwa mujibu wa taarifa, mafuriko hayo yameikumba mikoa ya Kusini-Mashariki mwa Taifa hilo la Ulaya.
Kutokana na athari za mafuriko hayo, wakazi katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Murcia wameokolowa na kuhamishwa.
Katika hatua nyingine, mamlaka ya hali ya hewa ya Hispania imetahadharisha kuwa maeneo mbalimbali yatapokea mvua kubwa za kiwango cha milimita 250–300.
Ikumbukwe, mwishoni mwa mwaka jana, Mji wa Valencia ulikumbwa na mafuriko makubwa zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo, ambapo watu takribani 200 walipoteza maisha.
Hata hivyo, historia inaonesha kuwa mvua zenye madhara makubwa nchini Hispania hutokea mara moja au mara mbili pekee ndani ya miaka 10.
Published:


