BOGOTA, Colombia
RIPOTI mpya ya Taasisi ya Global Witness imeitaja Colombia kuwa ndilo Taifa lenye idadi kubwa ya mauaji ya wanaharakati wa mazingira.
Kwa mwaka jana pekee, kwa mujibu wa kile kinachoelezwa na ripoti hiyo, wanaharakati 48 waliuawa nchini Colombia.
Aidha, ukiacha Colombia, mataifa mengine ya Latin Amerika yaliyotajwa kuwa tishio ni Guatemala yenye vifo 20 na Mexico yenye vifo 18.
Ni kwa maana hiyo, asilimia 80 ya wanaharakati 142 waliouawa mwaka jana duniani kote walikuwa katika Bara la Latin America.
Pia, ripoti imeeleza kuwa asilimia kubwa ya vifo hivyo ni vya wanaharakati wa mazingira katika maeneo ya migodi, uwindaji haramu na miradi ya nishati.
Kwa upande mwingine, idadi hiyo ya vifo 142 imeshuka kwa asilimia 28, ukilinganisha na takwimu za mwaka 2023, kwa mujibu wa Global Witness.
Published:


