5.7 C
New York

Ajali yaua wanafunzi kidato cha sita Rorya

Published:

Na Mwandishi Wetu,Gazetini

Watu saba wamefariki dunia wakiwamo wanafunzi wawili wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Songe, Musoma baada ya gari Toyota Succeed walilokuwa wakisafiria kugonga kwa nyuma Fuso lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya kuharibika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Mark Njera, ajali hiyo imetokea Kijiji cha Buganjo wilayani Rorya leo Septemba 11,2025 saa 11 alfajiri.

Amewataja wanafunzi hao kuwa ni Kwinta Gerald(18) Anitha Selemani(18). Wengine

walifariki ni Kelivin Orando(28), Ombura Ududo(34), John Abraham(30), Sharome Benard(30) wote wakazi wa Rorya.

Kamanda Njera amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni  ni mwendokasi wa  wa dereva wa gari aina ya Toyota Succeed kwa kuendesha bila kuchukua tahadhari.

Ameeleza kuwa dereva wa gari aina ya Mitsubish Fuso iliyokuwa  imeharibika na kupaki pembeni  mwa barabara ilichukua tahadhari  kwa kuweka  alama(reflective triangle).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img