Na Mwandishi Wetu, Gazetini
Bodi ya Wakurugenzi ya Taifa Group Limited, imetoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa hivi karibuni kuhusu miamala iliyofanywa na kampuni zetu tanzu za Tancoal Energy Limited (TANCOAL) na Williamson Diamonds Limited (WDL), zinahusu ununuzi wa hisa katika Tancoal na WDL.
Kwa mijibu wa Taarifa kwa Umma iliyotolewa naTaifa Group Limited, madai hayo hayana msingi wowote na ni upotoshaji, kwani miamala ambayo ilifanywa kwa kuzingatia sheria za nchi na za kimataifa kwa kuzingatia uwazi.




