13.1 C
New York

Wafanyakazi Shirika la Ndege Canada wagoma

Published:

TORONTO, Canada
WAFANYAKAZI wa Shirika la Ndege la Canada wameendelea na mgomo wakishinikiza ongezeko la mshahara.
Kwa mujibu wa Shirika hilo, mgomo huo wa wafanyakazi, wakiwano wahudumu, umetibua safari za abiria takribani 130,000 kwa siku moja.
Mbali ya kudai ongezeko la mishahara, pia wafanyakazi hao wanashinikiza malipo ya kazi wanazofanya pindi ndege inapokuwa haijaanza safari.
Kupitia taarifa yake, Shirika hilo lenye safari katika miji 180 duniani kote, lilieleza kuwa kwa sasa limesitisha utendaji.
“Shirika linasikitishwa na na athari za mgomo kwa wateja wetu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Ijumaa ya wiki hii, lilieleza kuwa limesitisha safari 623, sawa na kuathiri abiria zaidi ya 100,000 waliotarajia kutumia ndege za Shirika hilo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img