ISLAMABAD, Pakistan
WATU takribani 200 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko mjini Kashmir, Pakistan.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, likiwamo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mafuriko hayo yameua watu 194 ndani ya saa 24 tu.
Mbali ya vifo, mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali, zikiwamo nyumba 30.
Wakati wa jitihada za kuokoa, wahudumu watano wa helikopta nao waliripotiwa kupoteza maisha.
Kile kilichoelezwa na mamlaka ya hali ya hewa ya Pakistan ni kwamba mvua kubwa zitaendelea kunyesha hadi Agosti 21, mwaka huu.
Mvua zinazonyesha kuanzia Juni hadi Septemba ya kila mwaka nchini Pakistan ni robo tatu ya zile zinazonyesha Kusini mwa Bara la Asia.
Kwa msimu huu pekee, tayari watu zaidi ya 300 wamesharipotiwa kufariki kutokana na mvua kubwa nchini humo.
Published:


