6.4 C
New York

‘Met You’ ya Director P yapenya Afrika

Published:

Na Mwandishi Wetu

Mwimbaji na mwandaaji wa filamu mwenye asili ya Zambia na DR Congo anayeishi nchini Canada, Director P, amesema nyimbo yake mpya ya ‘Met You’ , imezidi kupenya kwa mashabiki zake barani Afrika tofauti na matarajio yake.

Director P, amesema wimbo huo uliotoka hivi karibuni akimshirikisha mwimbaji Ree mwenye asili ya Jamaica na Canada alitarajia utajipatia umaarufu ughaibuni peke yake lakini mashabiki wa Afrika wamevutiwa nao zaidi.

Akizungumza na gazetini.co.tz, Director P amesema huo ni ujio wake mpya wenye maudhui ya mapenzi na sasa yupo kwenye maandalizi ya kufanya video ili aendelee kuwapa raha mashabiki zake.

“Wimbo huu unahusu jinsi upendo unavyosikika unapozungumzwa kwa lugha nyingi, Ree alileta ladha ya Karibea kwenye kurekodi Met You, na mimi nimeleta ladha ya Afrika Mashariki jambo lililofanya wimbo uvutie mno hii ni zaidi ya hadithi ya mapenzi na muunganisho wa kitamaduni,” amesema Director P.
@@

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img