6.4 C
New York

Jonathan Budju kuachia ‘Ebenezer’ Julai 25

Published:

Na Christopher Msekena

Mwimbaji  nyota wa Injili kutoka nchini Canada, Jonathan Budju, amefanya hafla ya kusikiliza albamu yake fupi (EP),  Ebenezer itakayotoka mapema wiki ijayo Julai 25, 2025.

Jonathan Budju ni miongoni mwa waimbaji waliojipatia umaarufu mkubwa ughaibuni kwa mashabiki wa muziki huo uliogusa maisha ya watu hasa akitumia lugha ya kiswahili, kingereza na kifaransa kufikisha ujumbe.

Akizungumza na tuvuti hii, Budju amesema ndani ya EP hiyo kutakuwa na nyimbo kadhaa zenye mguso wa kipekee zitakazobadilisha maisha ya wengi hivyo anamwamini Mungu mashabiki watabarikiwa.

“Watu wachache wamesikiliza EP hii kwenye listening Party iliyofanyika hapa nyumbani Canada, mapokezi ni mazuri naamini itakapotoka hiyo Julai 25 itawabariki wengi na itapatikana kwenye digital platforms zote zinazouza na kupakuwa muziki duniani hivyo mashabiki wakati tayari,” amesema Jonathan Budju  a.k.a Son of God.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img