SEOUL, Korea Kusini
MVUA kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha raia zaidi ya 3000 kuyakimbia makazi yao katika maeneo mbalimbali ya Korea Kusini.
Jimbo la South Chungcheong ni miongoni mwa maeneo hayo yaliyoathirika na mvua hiyo ya siku nne mfululizo.
Aidha, taarifa zinaeleza kuwa tayari mvua hiyo imesababisha vifo vya watu wanne, huku wawili wakiwa hawajulikani walipo.
Kwa upande mwingine, mamlaka zimetahadharisha kuwa mvua hiyo itaendelea hadi Jumatatu ya keshokutwa.
Wakati huo huo, mvua hiyo imesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu, yakiwamo majengo zaidi ya 640, barabara 388 na mashamba 59.
Published:


