6.4 C
New York

Diddy aanza masomo akiwa gerezani

Published:

LOS ANGELES, Marekani
RAPA mwenye jina kubwa, P. Diddy, ameanza kuhudhuria darasa maalumu akiwa anaendelea kusota gerezani kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono.
Ripoti zinaeleza kuwa katika darasa hilo P. Diddy anafundishwa namna ya kuepuka unyanyasaji wa kingono, ikiwamo dhidi ya wanawake.
Ifahamike kuwa masomo hayo yanakuja ikiwa ni miezi mitatu pekee imebaki kabla ya hukumu yake katika makosa yanayomkabili.
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za burundani wa TMZ, pia mwanamuziki huyo anajifunza namna ya kuepuka matumizi ya dawa za kulevya.
Wakati huo huo, inaelezwa kuwa amekuwa akikutana ana kwa ana na wataalamu wa saikolojia, akiwamo Dk. Harry K. Wexler.
Huku hukumu ikisubiriwa Oktoba 3, tayari waendesha mashitaka wameiomba mahakama kumuadhibu P. Diddy kwa kifungo cha miaka minne.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img