13.9 C
New York

Haja ndogo isizidi sekunde 21 tu

Published:

LONDON, England
UMEWAHI kujiuliza huwa unatumia muda gani kumaliza haja ndogo unapoingia maliwato? Sasa, swali hilo lina maana kubwa mno kwa afya yako.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, kutumia chini au zaidi ya sekunde 21 ni dalili ya tatizo katika mwili wako.
Wataalamu wa Taasisi ya Teknolojia ya Georgia ya Marekani wanasema huwa inachukua wastani wa sekunde 21 kwa kibofu kumaliza kabisa haja ndogo iliyomo.
Endapo mtu atakuwa na wastani huo wa sekunde 21, basi atajisaidia haja ndogo mara nne hadi nane kwa siku, kwa mujibu wa wataalamu.
Kwamba endapo inakuchukua muda zaidi ya hizo sekunde 21, basi ni matokeo ya kukaa na haja ndogo kwa muda mrefu, jambo ambalo linaathiri kibofu.
Kuathirika kwa kibofu huko ni kukifanya kitanuke, tofauti na ukubwa wake wa kawaida wa mililita 400 hadi mililita 600.
Mfano sahihi katika hili ni tukio la mwaka 2020, ambapo mwanaume raia wa China alipasuka kibofu cha haja ndogo.
Hu (48), alipitiwa na usingizi kwa saa 18 alipotoka kunywa chupa 10 za bia. Kwa kutojisaidia haja ndogo kwa muda mrefu kutokana na usingizi, kibofu kikapasuka.
Pia, wanatahadharisha tabia ya kukaa na haja ndogo kwa muda mrefu wakisema inasababisha maambukizi ya kibofu na matokeo yake kuathiri moja kwa moja utendaji kazi wa figo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img