PYONGYANG, Korea ya Kaskazini
SERIKALI ya Korea ya Kaskazini imemtaka Balozi wa Uswis, Sylvain Astier, kuondoka nchini humo ndani ya saa 48.
Korea imekuja na uamuzi huo, pamoja na kuufunga ubalozi wa Uswis, zikiwa ni wiki chache tu tangu ulipofunguliwa.
Uamuazi huo umetokana na hatua ya awali ya Uswis kuiwekea vikwazo kambi ya Watoto wa Korea ya Kaskazini.
Uswis iliiwekea vikwazo kwa madai kuwa madai kuwa imekuwa ikitumika kuhamisha watoto wa Ukraine walioko kwenye maeneo yaliyochukuliwa na Urusi na kuwapeleka Korea Kusini.
Wakati huo huo, Uswis imekuwa ikiitaja kambi hiyo kutumika kuwaunganisha watoto wanaotoka Ukraine kwa kuwapa mafunzo.


