WASHINGTON DC, Marekani
SERIKALI ya Marekani imetangaza kuziongezea ushuru wa asilimia 20 bidhaa za nchi 14, zikiwamo za Umoja wa Ulaya, pamoja na China.
Hatua hiyo inakuja baada ya uchunguzi wa miezi nane uliofanywa na Marekani kubaini kile ilichokiita kutokuwapo kwa usawa wa kibiashara kati yao na nchi hizo.
Marekani imedai kuwa nchi hizo zimekuwa zikiingia bidhaa za bei rahisi, kiasi cha kuvinyima uhuru viwanda vyake vya ndani.
Aidha, China ni moja ya nchi hizo zilizowekewa ongezeko hilo la ushuru, kama ilivyo kwa Japan, Korea ya Kusini, Taiwan, na Malaysia.
Katika hatua nyingine, ‘adhabu’ hiyo imezikumba pia Bangladesh, Cambodia, India, Indonesia, Singapore, Uswis, Thailand na Vietnam.
Wakati huo huo, Mexico na Norway zimewekwa kando, huku Marekani ikieleza kuwa bado iko kwenye meza ya mazungumzo na mataifa hayo.


