22 C
New York

Trump akana kuisaidia Iran

Published:

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amekana madai ya kuiwezesha Iran kiasi cha Dola bilioni 30 ili kitumike katika mpango wa nyuklia.

Siku chache zilizopita, Shirika la Habari la CNN ndilo lililoripoti kuwa utawala wa Rais Trump umekubali kutoa fedha hizo ikiwa ni sehemu ya makubaliano kuwa Marekani itanufaika na madini ya uranium kutoka Iran.

Kwa upande wake, Rais huyo ameziita taarifa hizo kuwa ni uzushi unaopaswa kupuuzwa.

Tangu April, mwaka huu, Iran na Marekani zimekuwa kwenye mazungumzo yanayotajwa kulenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa hayo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img