13.1 C
New York

Sinema mpya yaanza  kuelekea mechi ya Dabi kesho, Simba yakimbia mkutano wa wanahabari

Published:

Na Mwandishi Wetu

Picha iliyotumwa na klabu ya Simba kwenye mitandao yao ya kijamii ni ujumbe  tosha baada ya kocha wao Fadlu Davis na nahodha wa kikosi hicho kushindwa kutokea katika mkutano wa wanahabari leo Juni 24,2025 kuzungumza  kwa mujibu wa kanuni kuelekea mchezo wa kesho  wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa.


Katika mkutano huo ambao Yanga ndiyo wenyeji, kama ratiba ilivyoonesha kocha wao Hamdi Miloud alifika kwa wakati akiwa na nahodha Dickson Job, wakazingumza na waandishi wa habari.

Picha ya Simba waliyotupia kwenye mitandao ya kijamii muda mfupi baada ya kukacha mkutano wa wanahabari leo Juni 24, 2025.

Baada ya kumaliza ilitakiwa kuwa zamu ya Simba lakini hakuna aliyeonekana  ambapo kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Karim Boimanda, wahusika hawapatikani kwenye simu.

Kutokana na hali hiyo,  Boimanda aliamua kufunga mkutano huo na kuwataka waandishi wa habari waondoke kwa sababu kuna shughuli nyingine zinatakiwa kuendelea kuliko kisubiri watu ambao hawajui nini kimewakuta.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hamdi Maloud akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo dhidi ya Simba kesho ambapo amesema wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Msimu 2024/25.

“Kwa mujibu wa ratiba ilitotumwa kwa klabu zote mbili, Simba ambaye ni mgeni katika mchezo huu alipaswa kuwepo hapa saa 5:30 kuanza mkutano,  lakini tumefanya jitihada kadhaa  bahati mbaya wahusika hawapatikani kwenye simu kwa hiyo tunashindwa kuelewa   changamoto  ni nini. Taarifa nyingine zitatolewa baadaye,” ameeleza Boimanda.

Ikumbukwe kuwa kumekuwa na  matukio mengi tangu mchezo huu ulipotangazwa kuchezwa Machi 8, 2025 ambapo  uliahirishwa baada ya Simba  kushindwa kufika uwanjani. Ukapangiwa tarehe nyingine Juni 15, Yanga nayo ikazua jambo kwa kutoa masharti ili icheze mchezo hadi kusababisha  baadhi ya viongozi wa Bodi ya Ligi kujiuzulu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img