17.4 C
New York

Aliyempiga mkwara Padri Kitima kabla ya kushambuliwa akamatwa

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na kumhoji Frey Edward Cossey ( 51) Mkazi wa Dodoma na Mbezi beach Makonde Dar es Salaam kufuatia chapisho lake la vitisho dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima alilolitoa kwenye mitandao ya kijamii kabla ya tukio kushambuliwa Padri huyo.

Akizungumza jijini leo Mei 05,2025, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema upelelezi wa shauri hilo unaendelea.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Frey April 28,2025 Cosseny  aliandika “Mwambieni Kitima iko siku ataingia kwenye 18 hatokaa asahau Tanzania muacheni ajifanye mwanasiasa. Mfikishieni message siku si nyingi atapata anachokitafuta dawa yake iko jikoni atakuja kuozea jela.”

Mtuhumiwa huyo anakuwa wa pili kutiwa mbaroni ikiwa siku tano zimepita tangu Padri  Kitima kushambuliwa Aprili 30, 2025 kwenye makazi yake Kurasini jijini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya baraza hilo na hadi sasa amelazwa Hospitali ya Aga Khan akiendelea kupatiwa matibabu.

Related articles

Recent articles