8 C
New York

Waziri Mkuu mpya kujulikana kesho

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho Alhamisi Novemba 13, 2025 katika Kikao cha tatu cha Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 kitakuwa na kazi mbili muhimu ambazo ni kuthibitisha jina la Waziri Mkuu na kumchagua Naibu Spika.

Hayo yameelezwa leo na Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu baada ya zoezi la Wabunge kula kiapo kumalizika.

” Kesho Alhamisi kikao cha tatu cha mkutano wa kwanza wa Bunge kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu, uchaguzi na kiapo cha Naibu Spika, wabunge wote wanaombwa wawepo kuanzia saa tatu kasoro dakika 10 kila mtu awepo kwenye kiti chake,’ amesema.

Bunge  la 13 lilianza Jumanne, Novemba 11, 2025, likianza na uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha kiapo cha uaminifu na ahadi ya uzalendo kwa wabunge wateule, zoezi ambalo limehitimishwa siku ya leo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa), uteuzi wa Waziri Mkuu hufanyika kwa kufuata utaratibu maalum unaoanza mara baada ya Rais kuapishwa rasmi kushika madaraka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img