5.7 C
New York

Watanzania wahimizwa kushiriki mchezo wa kuogelea bila kujali umri

Published:

Na Winfrida Mtoi, Gazetini

Watanzania wamehimizwa kushiriki na kujifunza mchezo wa kuogelea bila kujali umri ili kulinda afya na kutengeneza mahusiano na watu tofauti ikiwamo kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Elimu na Maendeleo wa Chama Cha Kuogelea  Tanzania (TSA),  Jeremiah Keema wakati wa mashindano ya mchezo huo kwa watu wazima ‘Masters’, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita  jijini Dar es  Salaam.

Keema ambaye pia ni kocha wa mchezo huo, amesema mtu anaweza kushiriki mashindano ya Mastars hata akiwa na umri wa miaka 100, na yule anayetamani na hajui kuogelea wana uwezo  kumfundisha akafanikiwa.

“Kwa mimi nikiwa mmoja wa viongozi wa Swimming Tanzania, nawakaribisha watu wote, umri wowote hasa kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea hata akiwa na 100, hawa ni watu wazima wanaweza kushiriki mashindano ya Masters. Mashindano si kwa ajili tu ya kushinda, pia kushirikiana mambo kadhaa ikiwamo ya kijamii,” ameeleza Keema.

Ameeleza kuwa Tanzania ipo katika kiwango kizuri cha ushiriki wa mashindano ya Masters, ikishika namba mbili kwa Afrika Mashariki ambapo inayoongoza ni Kenya.

Kuhusu mashindano yaliyofanyika amesema lengo lilikuwa ni maandalizi ya mashindano yanayotarajia kufanyika nchini Kenya mwezi ujao.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img