10.7 C
New York

Utafiti: Wasiopiga mswaki hatarini kupata saratani

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

BAKTERIA wa kinywani wanaoweza kuondoshwa kwa kupiga mswaki husababisha saratani ya kongosho, kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani. Kwa miaka mingi, wataalamu wa afya wamekuwa wakieleza umuhimu wa usafi wa kinywa, pia wakisema una mchango mkubwa katika kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Sasa, kwa mujibu wa utafiti mpya wa Idara ya Afya ya Chuo Kikuu cha New York, mate yanaweza kusafirisha bakteria hatari wa kinywani hadi kwenye kongosho na kusababisha saratani.

Mmoja wa wataalamu waliofanya utafiti huo, Dk. Richard Hayes, kupitia andiko lake kwenye jarida la JAMA Oncology, anasema usafi wa kinywa kwa kupiga mswaki si tu huzuia magonjwa ya meno, bali pia ni kinga dhidi ya saratani.

Kwa upande wake, Dk. Yixuan Meng, ambaye ndiye kiongozi wa utafiti, anasema: “Majibu ya utafiti wetu yanatoa picha mpya ya uhusiano mkubwa uliopo kati ya bakteria wa kinywani na ugonjwa wa saratani ya kongosho.”

Dk. Yixuan anaongeza kuwa mbali ya uvutaji wa sigara na umri mkubwa, pia afya ya kinywa inaweza kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa huo. Kwa mujibu wa msomi huyo, baadhi ya bakteria hatari wa kinywani, ambao husababisha saratani ya kongosho, pia husababisha magonjwa ya meno kutokana na uwezo wake wa kutafuna tishu.

Saratani ya kongosho ni miongoni mwa magonjwa hatari duniani, ukitajwa kusababisha vifo zaidi ya 10,000 kila mwaka. Kuziweka sawa takwimu, hiyo ni sawa na kifo kimoja kila baada ya dakika 60. Idadi ya vifo inatarajiwa kufikia 201,000 mwaka 2040.

Changamoto kubwa ya saratani ya kongosho ni kwamba dalili zake kujitokeza wakati ugonjwa huo ukiwa umefikia hatua mbaya zaidi. Mbaya zaidi, wakati ugonjwa huo ukionekana kuwa ni wa wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 75, vijana nao wamejikuta wakinasa katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa utafiti wa mwaka jana wa Daily Mail, kasi ya kundi la vijana kupata saratani ya kongosho imeongezeka kwa asilimia 200, huku wasichana wenye umri chini ya miaka 25 wakiwa hatarini zaidi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img