4 C
New York

Cole amchongea Martinez kwa mabosi United

Published:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Chelsea, Joe Cole, anaamini ni wakati sahihi sasa kwa uongozi wa Manchester United kumfungulia mlango wa kutokea beki wa kati raia wa Argentina, Lisandro Martinez.

Cole ameibuka na kauli hiyo baada ya Martinez kuonesha kiwango kisichoridhisha katika mchezo waliotandikwa mabao 2-0 na Chelsea jana Oktoba 31, 2026 kwenye mchezo wa Ligi uliochezwa Stamford Bridge.

Kipigo hicho kimeiacha Man United ikiwa haijaonja ushindi katika mechi tisa mfululizo, mwenendo unaomuweka pabaya kocha Michael Carrick.

Martinez analaumiwa kwa kushindwa kumdhibiti Morgan Rogers aliyeifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya tano tu baada ya mapumziko.

Dakika nne baadaye, mlinzi huyo alijikuta tena kwenye shida baada ya kumchezea rafu Wesley Fofana na kuipa Chelsea mkwaju wa penalti. Martinez alilimwa kadi nyekundu.

“Kwa vyovyote Manchester United itakavyokuwa, nafikiri Lisandro Martinez amemaliza. Tunajua mafanikio yake akiwa na Argentina lakini kwa Manchester United naona inatosha,” amesema Cole.

Related articles

Recent articles