5.7 C
New York

Kidao aondolewa  TFF

Published:

Na Mwandishi Wetu

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Kidao Wilfred.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 24, 2025 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, mkataba wa Kidao unafikia tamati Septemba 30 mwaka.

“Uteuzi wa Mirambo ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, utaanza rasmi tarehe 1 Oktoba 2025,” imesema taarifa hiyo.

Kidao amedumu katika nafasi hiyo miaka nane, kwa mara ya kwanza  aliteuliwa mwaka 2017, hivyo kukaa  kwenye kiti hicho kwa mihula mitatu tofauti ya uongozi wa Rais wa TFF, Wallace Karia.

Oscar Mirambo

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img