Na Mwandishi Wetu, Gazetini
MSANII wa kizazi kipya mwenye makazi yake Atlanta, Marekani, Dogo Red, ametamba kutikisa Afrika Mashariki na video ya wimbo Vanessa aliowashirikisha wasanii wa Burundi Wiz Designer na Rich Forever.
Dogo Red ni miongoni mwa wasanii wachache wapambanaji waliotokea Afrika Mashariki wanaoendelea kufanya muziki ughaibuni kwa mafanikio na Ijumaa hii anaachia kolabo hiyo.
Akizungumzia kolabo hiyo Dogo Red ambaye ni bosi wa Wapamba Classic , amesema audio ya wimbo huo ilipokewa kwa kishindo na mashabiki katika mitandao mbalimbali ya kusikiliza muziki duniani na kiu yao sasa ni kuona video ya Vanessa ikitoka.

“Nimejibu kiu ya mashabiki wa Dogo Red kwa kuachia hii video, nitaiachia Ijumaa hii kwenye chaneli yangu ya YouTube hivyo mashabiki zangu na wale wa Wiz Designer na Rich Forever tutakata kiu yao ya muda mrefu,” amesema Dogo Red.


