13.9 C
New York

Raia kumiliki silaha kunavyoitesa Marekani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
KATIKA kila raia 100 wa Marekani, kuna bastola 120. Hiyo ni kwa mujibu wa utafiti wa Taasisi ya SAS ya nchini Uswis. Ni kiwango cha juu zaidi duniani, kwa raia kumiliki silaha.
Kwamba Marekani inaingoza, ikifuatiwa na Argentina, ambayo katika kila raia wake 120, kuna bastola 62. Ni takribani nusu ya Marekani.
Taifa jingine na linaloshika nafasi ya tatu kwa kiwango kikubwa cha raia wake kumiliki silaha hiyo ni Yemen. Bastola 53 katika kila watu 100.
Kwa mujibu wa tafiti, kati ya bastola milioni 857 zinazomilikiwa na raia duniani, milioni 395 (46%) ziko Marekani, ambapo asilimia 44 ya watu wazima wanamiliki.
“Idadi kubwa hiyo inatokana na ilivyo rahisi kwa raia wa Marekani kumiliki bastola. Kwa ufupi, ni haki ya Kikatiba kwa kila mtu kuwa nayo,” anasema Profesa wa Chuo Kikuu cha Texas, Zachary Elkins.
Kutokana na Katiba, uhitaji wa bastola ni mkubwa. Mwaka 2018, bastola milioni tisa zilitengenezwa na kuingia sokoni. Ni mara mbili ya zilizokuwapo mwaka 2008.
Ni tofauti na mataifa mengine ya Amerika, mathalan Mexico, licha ya kwamba nayo yana idadi kubwa ya raia wanaomiliki silaha.
Mathalan, Mexico ni moja ya mataifa yanayopinga umiliki holela wa silaha kwa raia wake. Ni duka moja pekee linalouza bastola nchini humo.
Kwa Marekani, mtazamo ni kwamba kiwango kikubwa cha umiliki wa silaha kwa raia kutapunguza matukio ya uhalifu. Ni kweli?
Hata hivyo, mtazamo huo unapingana na tafiti za hivi karibuni, nyingi zikionesha kuwa Marekani ina vifo vingi vitokanavyo na bastola kuliko mataifa mengine makubwa.
Mfano; Wamarekani zaidi ya 23,000 walijiua kwa kujipiga risasi mwaka 2019. Ni asilimia 44 ya vifo vyote vya bastola duniani.
Ni mara nane ya Canada inayoshika nafasi ya saba duniani kwa idadi kubwa ya raia wanaomiliki silaha. Ni mara 22 ya taifa lolote la Umoja wa Ulaya (EU) na ni mara 23 ya Australia.
Tafiti zinafafanua zaidi, kwamba vifo vya bastola katika Jimbo moja tu la Marekani, Washington DC, ni vingi kuliko vinavyotokea Brazil.
Wakati Serikali ya Mexico ilipokamata bastola zinazomilikiwa na raia kinyume cha sheria mwaka 2019, ilibaini kuwa asilimia 68 ni aidha zilitengenezwa au kuagizwa kutoka Marekani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img