27.2 C
New York

Chelsea yanasa mwingine, yafikisha saba 

Published:

LONDON, Uingereza 

KLABU ya Chelsea imemtambulisha beki wa pembeni kutoka Rayo Vallecano ya Hispania, Pep Chavarria.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na Chelsea majira haya ya kiangazi.

Chavarria anaingia kikosini kuziba pengo la Marc Cucurella, ambaye wiki chache za hivi karibuni alijiunga na vigogo wa La Liga, Real Madrid.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza na Hispania, mchezaji huyo ameigharimu Blues kitita cha Pauni milioni 16.3.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Chavarria amesema: “Nimefurahi kuwa hapa. Ni ndoto yangu kwa sababu Chelsea ni moja ya klabu kubwa duniani.”

Related articles

Recent articles