27.2 C
New York

Ronaldo afunga ndoa na Georgina

Published:

LISBON, Ureno

BAADA ya miaka 10 ya uchumba, hatimaye staa wa soka, Cristiano Ronaldo amefunga ndoa na mpenzi wake, Georgina Rodriguez.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Ronaldo ndiye aliyeposti picha ya harusi yao iliyofungwa nchini Ureno.

Katika picha hiyo, ameposti mkono wake ukiwa juu ya wa bibiye huyo, huku yote ikiwa na pete za ndoa.

Kwa upande wa vyombo vya habari vya Ureno, vimeiita kuwa ni ‘ndoa ya mwaka’ na kueleza kwamba ilifungwa jana Agosti 11, 2026, mjini Lisbon.

Aidha, vyombo vya habari hivyo vilidai kuwa hafla ya ndoa hiyo ilihudhuriwa pia na watoto watano wa Ronaldo na Georgina.

Related articles

Recent articles