LONDON, England
HIYO ni kwa mujibu wa wakongwe wa Ligi Kuu ya England (EPL), Jamie Carragher na Gary Neville, ambao kwa sasa ni wachambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha Sky Sports.
Kwa upande wake, lejendari wa Liverpool, Carragher, anaamini timu yake hiyo ina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa waliobeba msimu uliopita.
Neville, ambaye ni beki wa zamani wa Manchester United, anaiona Arsenal ya kocha Mikel Arteta ikiwa na nafasi kubwa zadi safari hii.
Hata hivyo, wakongwe hao wanakubaliana kuwa Manchester City ni miongoni mwa timu zenye jeuri ya kutwaa taji hilo msimu huu.
Akiizungumzia Arsenal, Neville alisema: “Bado nipo na timu ambayo imekuwa bora mno kwa misimu mitatu ya hivi karibuni, Arsenal.”
Neville aliongeza kuwa usajili wa mpachikaji mabao kutoka Sporting Lisbon, Viktor] Gyokeres, utaipaisha zaidi Arsenal katika mbio za ubingwa.
Carragher, licha ya kuitabiria ubingwa Liverpool, alisema Chelsea inaweza kumaliza ndani ya ‘Top Four’ na kukata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Kwa upande mwingine, wachambuzi hao walikubaliana kuwa itakuwa ngumu kwa Newcastle United kutwaa ubingwa, na badala yake itamaliza ndani ya nafasi sita za juu kwenye msimamo wa EPL.
Pia, Neville alitabiri kuwa Ruben Amorim wa Man United ndiye kocha atakayefanya vizuri msimu huu, wakati Carragher alitupa karata yake kwa Oliver Glasner aliyeipa Crystal Palace taji la FA wiki chache zilizopita.
Published:


