28.7 C
New York

Dawa za kulevya ‘zamaliza’ vijana Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani

IDADI ya vifo vya vijana vitokanavyo na utumizi wa dawa za kulevya imeripotiwa kuongezeka kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja nchini Ujerumani.

Kwa mwaka 2025, vijana waliopoteza maisha kwa magonjwa yatokanayo na dawa za kulevya walifikia 2,150.

Kwa mujibu wa Kamishina wa Dawa za Kulevya wa Ujerumani, Hendrik Streeck, idadi hiyo imeongezeka kutoka 2,137 mwaka 2024.

Aidha, vifo vinavyotokana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya cocaine imetajwa kuongezeka kwa asilimia 110.7, ikilinganishwa na mwaka 2021.

Hata hivyo, bado idadi ya vifo 2,150 kwa mwaka 2025 ni ndogo, ikilinganishwa na vifo 2,227 kwa mwaka 2023.

Streeck amesema kuongezeka kwa idadi ya vifo vya vijana kumetokana na kundi hilo kutokufahamu madhara ya utumizi wa dawa za kulevya.

Kwa upande mwingine, ametaja msongo wa mawazo kuwa moja ya sababu za vijana kujitumbukiza katika matumizi ya dawa hizo.

Kuthibitisha hilo, Lorant mwenye umri wa miaka 46 anasema aliingia kwenye ‘unga’ ili kukwepa msongo wa mawazo uliompa mawazo wa kujiua.

Related articles

Recent articles