28.7 C
New York

Arsenal yang’oa nahodha Madrid

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili wa nahodha wa timu ya wanawake ya klabu ya Real Madrid, Misa Rodriguez.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, ni kipa ambaye ameondoka Madrid akiwa amemaliza mkataba wake.

Misa anatua Arsenal kuwania namba mbele ya Daphne Van Domselaar, Anneke Borbe na Isabella Damm.

Ni miongoni mwa wachezaji wazoefu ndani ya Madrid, akiwa amecheza mechi 215, pia akicheza 24 katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.

Anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na Arsenal majira haya ya kiangazi baada ya Damm, Georgia Stanway, Geraldine Reuteler, Selina Cerci, Ona Batlle na Lisa Baum.

Wakati huo huo, Misa anakuwa wa tano kutua Emirates akiwa mchezaji huru baada ya Stanway, Batlle, Cerci na Reuteler.

Related articles

Recent articles