14.7 C
New York

Njaa yaua binti wa miaka minne

Published:

JERUSALEM, Israel
HUKU vita ikiendelea, binti mwenye umri wa miaka minne, Razan Abu Zaher, amepoteza maisha kutokana na njaa kali inayowakumba wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madaktari, binti huyo alifariki akiwa hospitali.
Razan anakuwa mmoja ya Watoto 76 waliopoteza maisha kwa njia hiyo, wakati huu Israel ikiendelea kuishambulia Palestina.
Mwezi uliopita, kituo cha runinga cha CNN kilifanya mahojiano na mama yake mzazi, Tahrir Abu Daher, ambaye alikiri kutokuwa na fedha za kununua chakula.
Aidha, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limeeleza kuwa sehemu kubwa ya vifo hivyo imetokana na uamuzi wa Israel kuzuia misaada inayoingia Gaza.
Katika siku tatu za hivi karibuni, Razan anakuwa mtoto wa tatu kufariki kwa njaa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img