28.1 C
New York

Mambo ni moto msimu mpya Ligi Kuu za Ulaya: La Liga

Published:

MADRID, Hispania

MSIMU mpya wa La Liga (2026-27) utaanza kesho, yaani Jumamosi ya Agosti 15, ambapo Alaves itafungua pazia kwa kuikaribisha Getafe.

Gumzo ni kurejea kwa Jose Mourinho katika viunga vya Santiago Bernabeu. Ni kocha aliyewahi kuipa Madrid mataji matatu (La Liga, Copa del Rey na Spanish Super Cup).

Mourinho amerudi baada ya miaka 13 tangu alipoondoka klabuni hapo. Amesajili nyota wanne kuimarisha kikosi, ambao ni mabeki Marc Cucurella, Ibrahima Konate na Denzel Dumfries, kiungo Bernardo Silva, na mshambuliaji Yan Diomande.

Vinicius Junior aliyekuwa akihusishwa na Arsenal amebaki kikosini, hivyo ataendelea kushirikiana na Kylian Mbappe na Jude Bellingham.

Swali ni je, Mourinho ataimudu kumaliza vita ya ustaa kikosini, ambapo baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa, mathalan Mbappe na Vinicius, walikuwa hawaelewani?

Pili, Mourinho atarejesha makombe Santiago Bernabeu? Kwa misimu miwili mfululizo, taji la La Liga limetua kwa wapinzani wao, Barcelona, licha ya Madrid kuwa na wachezaji bora zaidi.

Kwa upande wa Barcelona, wamepoteza mpachikaji mabao wao hatari, Robert Lewandowski, lakini wameziba pengo lake kwa usajili wa nyota wawili, Anthony Gordon na Karim Adeyemi.

Atletico Madrid, kama kawaida yao, wataipambania ‘Top Three’, huku ushindani mkali ukitoka kwa Villarreal na Real Betis.

Related articles

Recent articles