9 C
New York

Kenya yajitoa  mashindano ya  CECAFA 

Published:

Na Mwandishi Wetu

Timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ imejiondoa katika mashindano maalumu ya CECAFA  yaliyopangwa kuanza leo Julai 21,2025 jijini Arusha  kwa ajili  ya maandalizi ya   michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN- 2024).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la  Soka nchini Kenya (FKF), uamuzi huo umefanyika kutokana na  mapendekezo na ushauri wa benchi la ufundi la timu hiyo, likiongozwa na Kocha Mkuu Benni McCarthy, baada ya tathmini ya kina ya hali iliyopo kwa sasa, ikiwamo kutoridhishwa na mazingira.

Kenya ilikuwa icheze leo dhidi ya Uganda lakini baada ya kujitoa, itarejea nchini Kenya na kuendelea na maandalizi ya CHAN.

Mashindano hayo maalum yalikuwa yashirikishe  nchi nne za Tanzania, Uganda, Senegal na Kenya.

Michuano ya CHAN inatarajiwa kuanza  Agosti 2, 2025 ambapo Tanzania itafungua   dimba dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. 

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img