MOSCOW, Urusi
ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi wa Urusi, Roman Starovoit, amefariki, huku mwili wake ukikutwa na jeraha la risasi.
Wakati huo huo, kile kilichoelezwa na Kamati ya Uchunguzi kupitia taarifa yake ya awali, ni kama Starovoit alijiua.
Ikumbukwe, taarifa za kifo chake zimekuja zikiwa ni saa chache tu baada ya mwanasiasa huyo ‘kutumbuliwa’ na Rais Vladimir Putin.
Aidha, kwa mujibu wa vyanzo vya habari, baada ya kung’olewa, Starovoit angefunguliwa kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma.
Starovoit aliteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi Mei, mwaka jana, na kabla ya hapo alihudumu kwa miaka sita katika nafasi ya Gavana wa Jimbo la Kursk.
Published:


