13.1 C
New York

TSA yateua waogeleaji wa kuiwakilisha Tanzania Aquatics Kanda ya III

Published:

Na Mwandishi Wetu

Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), kimefanya uteuzi wa awali wa waogeleaji watakaoshiriki Mashindano ya Africa Aquatics Kanda ya III, yatakayofanyika Oktoba 16-19, 2025, Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya TSA, kikosi hicho kinajumuisha waogeleaji wenye vipaji kuanzia umri wa miaka 11 na kuendelea, pia timu itajumuisha waogeleaji wakongwe (masters).

Imeeleza kuwa orodha rasmi ya wanamichezo hao itatolewa baada uthibitisho wa upatikanaji wa waogeleaji hao kutoka kwa wazazi au walezi wao.

“Ili kuhakikisha kuwa wanaogeleaji waliochaguliwa wako katika hali bora kwa ajili ya mashindano, timu ya ufundi ya TSA inapanga kuanzisha kambi kali ya mazoezi ya mchana, itakayoanza Agosti 2025. Kambi hii itatoa maandalizi kamili chini ya uongozi wa makocha wakuu wa kitaifa,” imesema taarifa hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img