ANKARA, Uturuki
VIONGOZI watatu wa chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Taarifa zaidi zinawataja waliokamatwa kuwa ni mameya wa majimbo ya Adana (Zeydan Karalar), Antalya (Muhittin Bocek) na Adiyaman (Abdurrahman Tutdere).
Kwa miezi kadhaa, mamlaka za Uturuki zimekuwa zikiendesha ‘kamatakamata’ ya wanasiasa wa chama cha upinzani, Republican People’s Party (CHP).
Itakumbukwa,Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu, ambaye pia ni mkosoaji mkubwa wa Rais Recep Tayyip, ni miongoni mwa waliowahi kushikiliwa.
Itakumbukwa, kukamatwa kwa Imamoglu mwanzoni mwa mwaka huu kuliibua maandamano makubwa Zaidi kuwahi kutokea ndani ya miaka 10 ya hivi karibuni.
Kwa sasa, kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, tayari viongozi watatu wa CHP wanashikiliwa.
Published:


