LONDON, England
KIUNGO wa Arsenal na timu ya taifa ya Ghana, Thomas Partey, ameshitakiwa kwa kosa la kubaka.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Partey alifanya hivyo kati ya mwaka 2021 na 2022.
Inaelezwa kuwa mashitaka hayo yanahusisha wanawake watatu, ingawa Partey amekana kuhusika.
Partey mwenye umri wa miaka 32, alimaliza mkataba wake na Arsenal mwanzoni mwa wiki hii.
Nyota huyo alijiunga na Arsenal mwaka 2020 akitokea kwa vigogo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Atletico Madrid.
Msimu uliopita, alicheza mechi 35 na kufunga mabao manne, wakati Arsenal ilipomaliza ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Published:


