3.7 C
New York

Bado hakijaeleweka, Yanga yakomaa haichezi dabi Juni 15

Published:

Na Mwandishi Wetu

Licha ya kufanya kikao na uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), leo Juni 9, 2025, Klabu ya Yanga imeendelea  kushikilia msimamo wake kuwa haitacheza  mechi  ya Juni 15,2025 dhidi ya Simba endapo  hawatakapotimiziwa matakwa yao.

Kikao hicho kimefanyika ikiwa zimebaki  siku sita pelee kufikia tarehe ya mchezo huo ambao awali ulitakiwa kuchezwa Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. 

Kwa mujibu wa taarifa  iliyotolewa na Kamati ya Utendaji ya Yanga leo, imesema kuwa msimamo wao hautobadilika hadi pale mahitaji yao yatakapotimizwa.

Akizungumzia yaliyojili katika kikao hicho, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo, amesema kuwa kikao cha leo kilikuwa kwa ajili ya kupokea matakwa ya Yanga ambayo ni manne, kujiuzulu kwa Mwenyeketi wa bodi ya ligi, kujiuzulu kwa Ofisa mtendaji mkuu wa, Katibu mkuu wa Tff na kuona bodi ya ligi kuu inakuwa chombo huru.

“Hivyo basi matakwa hayo yamepokewa na yatawasilishwa kwa shirikisho la soka nchini TFF, ila kwa mamlaka ya bodi ya ligi mpaka sasa ni mchezo upo pale pale juni 15,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img