10.6 C
New York

Xi, Trump na Putin wakubaliana kuidhibiti ICC

Published:

BEINJING, China

RAIS wa China, Xi Jinping, amekuwa mwenyeji wa kikao kilichomkutanisha na marais wa Marekni, Donald Trump, na Vladimir Putin wa Urusi jana Novemba 19, 2028 mjini Shenzhen.

Katika hatua nyingine, viongozi hao walijadili na kukubaliana juu ya mabadiliko yanayopaswa kufanyika ndani ya Umoja wa Mataifa [UN], pamoja na kudhibiti mamlaka ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu [ICC].

Xi ameyaita mazungumzo yao kuwa ni msingi, akisisitiza kuwa yalijikita katika maeneo nyeti ya vita dhidi ya silaha za nyuklia, utawala bora, mgogoro wa Ukraine, na ulinzi dhidi ya nishati.

Mazungumzo hayo pia yaligusia jitihada za pamoja zinazopaswa kuchukuliwa na mataifa matatu hayo katika kuongeza usambazaji wa mafuta kwenye soko la dunia ili kuondosha uhaba uliopo.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wamesema Rais Putin, ambaye anapingwa na mataifa ya Ulaya kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine, amenufaika zaidi na mkutano huo kwani umeutumia kutuma ujumbe kwamba bado anakubalika mbele ya Marekani na China.

Related articles

Recent articles