MADRID, Hispania
REAL Madrid inajiandaa kumrejesha kikosini mshambuiaji wake wa zamani anayefanya vizuri Ligi Kuu ya Italia [Serie A], Nico Paz.
Paz ni miongoni mwa wachezaji wanaoibeba Como ya kocha Cesc Fabregas na alijiunga na klabu hiyo msimu wa 2024-25 baada ya kushindwa kupata uhakika wa namba Santiago Bernabeu.
Hata hivyo, katika mkataba wa awali na Como, kilikuwepo kipengele kinachoiruhusu Madrid kumsajili wakati wowote kwa ada ya euro milioni tisa.
Madrid waliposhindwa kufanya hivyo, Como ilimsajili moja kwa moja kwa ada ya euro miolioni 60 na sasa Wahispania hao watalazimika kulipa zaidi ili kumrusisha La Liga.
Lakini, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Hispania, bado hakuna ofa rasmi waliyotuma Madrid kwenda Como juu ya usajili Muargentina huyo.


