WASHINGTON DC, Marekani
KWA mujibu wa utafiti wa Taasisi ya Pew Research Center ya Washington, Marekani, idadi ya waumini wa Dini ya Uislam itakuwa kubwa kuliko wenzao, Wakiristo, ifikapo mwaka 2035.
Aidha, kwa takwimu za mwaka 2020, ilielezwa kuwa Wakiristo duniani kote ni bilioni 2.27, wakati Waislam walikuwa bilioni 2.02.
Hata hivyo, utafiti wa Pew umeeleza kuwa ongezeko la Waislam linatokana na idadi ya watoto kwenye familia zao.
Mathalan, Pew wamebaini kuwa wanawake wa Kiislam walikuwa na wastani wa kuwa na watoto 3.1 kati ya mwaka 2020 na 2025, ikilinganishwa na watoto 2.5 kwa wenzao wa Kikiristo.
Hivyo, kwa makadirio ya Pew kwa mwaka 2035, Waislam duniani kote wanatarajiwa kufikia bilioni 2.57, huku Wakiristo wakiwa ni bilioni 2.52.
Na endapo idadi itakuwa hivyo, Waislam watafikia bilioni 3.6 mwaka 2070, wakati Wakiristo watakuwa bilioni 3.


