MERSEYSIDE, Uingereza
KLABU ya Liverpool iko kwenye hatua nzuri ya kumsajili kiungo wa Monaco, Lamine Camara, kupitia usajili wa kiangazi, mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa ripoti, tayari yameshafanyika mazungumzo kati ya Liverpool na wawakilishi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal.
Chelsea walikaribia kumsajili Camara wakati wa kiangazi, 2026, lakini dili hilo liliota mbawa dakika za mwisho na mchezaji huyo kubaki Ligue 1.
Sasa, taarifa zinaeleza kuwa Liverpool wako mstari wa mbele baada ya mabosi wa Blues kuamua kuachana na mpango wa kumsajili.
Inaelezwa kuwa Chelsea wametemana naye na sasa wanaelekeza nguvu kwa kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, au Martin Zubimendi wa Arsenal.
Katika hatua nyingine, zipo ripoti zinazodai kuwa klabu zingine kubwa za Manchester United, Real Madrid na Bayern Munich nazo zinamtaka nyota huyo mwenye thamani ya euro milioni 70.


