16 C
New York

Kounde kuondoka Barca, asubiriwa Chelsea

Published:

CATALUNYA, Hispania

BEKI wa pembeni wa Barcelona, Jules Kounde, anatarajiwa kuondoka klabuni hapo kupitia dirisha dogo la Januari, 2027, kwa mujibu wa mtandao wa Football Insider.

Mlinzi wa kulia huyo anataka kuondoka Catalunya baada ya kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza. Ameanza katika mechi tatu tu za La Liga msimu huu.

Chelsea wamekuwa wakimfuatilia Mfaransa huyo kwa muda mrefu kwani walitaka kumsajili mwaka 2022 lakini aliamua kujiunga na Barcelona.

Aidha, Kounde [28], pia anaripotiwa kuingia kwenye rada za klabu nyingine kongwe ya jijini London, West Ham United.

Wakati huo huo, Chelsea imeitaka Manchester City kuweka mezani kitita cha Pauni milioni 70 kama inataka kumsajili beki wake mwenye umri wa miaka 23, Malo Gusto.

Related articles

Recent articles