16 C
New York

Taifa Stars hoi mkiani kufuzu AFCON 2027

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaburuza kwenye Kundi L ikiwa haina ushindi, na badala yake imekusanya pointi mbili tu baada ya kupata sare mbili.

Katika Kundi hilo la mechi za kufuzu AFCON 2027, Guinea-Bissau iko kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 10, ikiizidi tatu Nigeria inayoshika nafasi ya pili.

Guinea-Bissau wamefikisha pointi 10 hizo baada ya kuifunga Madagascar mabao 2-0 katika mechi ya jana Novemba 17, 2026, siku ambayo Nigeria na Stars zilitoka suluhu [0-0] Visiwani Zanzibar.

Nigeria ina pointi saba, huku kila timu ikiwa imeshacheza mechi nne na kubakiza mbili ili kuhitimisha mchakato wa kufuzu.

Madagascar iko nafasi ya tatu, ambapo kama ilivyo Tanzania, nayo haijashinda hata mechi moja kati ya nne ilizocheza.

Related articles

Recent articles