10.6 C
New York

Kofi Olomide: Dansa alivyovunja ndoa yake ya miaka 27 – [6]

Published:

KINSHASA, DRC

KATIKA maisha yake, Koffi ameona mara tatu lakini ana anaripotiwa kuwa na watoto 11 hadi 20 katika mahusiano yake na wanawake tofauti. Mkewe wa kwanza ni Marianne Makosso, ambaye alibahatika kupata naye watoto wawili.

Katika ndoa yake ya pili na Stephanie Godee, alipata watoto watatu, kisha kumuoa Aliane, ambaye ni mwanamitindo wa zamani wa Ufaransa, aliyeanza kutoka naye katika miaka ya 1990 jijini Paris, kabla ya kufunga ndoa Aprili 15, 1994, na kupata watoto watatu.

Kama itakumbukwa, Aliane ni mwanamke ambaye Koffi alimuimba katika nyimbo zake nyingi, zikiwamo ‘Miss des Miss’ [1993], ’12eme Dan’ [2012] na hata ‘Alidor’ [2017].

Binti yao, Didi-Stone Naike, ni mwanamitindo mwenye umaarufu mkubwa kwani amefanya kazi na majarida ya Vogue, Grazia na Vanity Fair. Kama hiyo haitoshi, alikuwa balozi wa Siku ya Wanawake ya Shirika la Watoto mwaka 2022.

Baada ya miaka 27 ya ndoa, Aliane alidai talaka mwaka 2021, chanzo kikitajwa kuwa ni tabia ya Koffi ‘kuchepuka’ na warembo wengine, hasa binti aliyekuwa naye kwenye bendi, Cindy Le Coeur.

Miaka miwili baada ya talaka, Koffi aliweka wazi kuwa kwa sasa anatoka kimapenzi na bibiye Cindy. “Nina miaka 30 tu iliyobaki kuishi, nataka kufia mikononi mwa Cindy Le Coeur,” alisema.

Tangu hapo, Koffi na Cindy aliyejiunga na Quartier Latin International mwaka 2007 akiwa mwimbaji, mrembo huyo kupandishwa cheo na kuwa dairekta, wameendelea kuwa na ukaribu uliodumu hadi leo.

Mwaka 2017, ziliibuka ripoti kuwa Cindy na Koffi wamepata mtoto, ingawa hakuna mmoja wao aliyejitokeza na kuthibitisha. Mwaka 2025, video iliyopostiwa TikTok ilionesha kile kilichotajwa kuwa ni sherehe ya ndoa yao.

Baadaye, Cindy alifichua kuwa walifunga ndoa ya asili mwaka 2008, kabla ya kufanya sherehe Februari 28, 2026, jijini Kinshasa.

Itaendelea …

Related articles

Recent articles