17.8 C
New York

Kigogo akimbia nyumbani kwake akiihofia Iran

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

KATIBU Mkuu wa Hazina nchini Marekani, Scott Bessent, amelazimika kuihama nyumba yake kutokana na tishio la kuuawa na Iran.

Taarifa za uhakika, kwa mujibu wa BBC, zinaeleza kuwa amehama nyumbani kwake Washington DC na sasa anaishi kwenye kambi ya jeshi.

Bessent amekuwa mstari wa mbele katika kampeni ya Marekani kutaka Iran itengwe na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni, mamlaka za usalama za Marekani zimedai kuwa Iran imekuwa ikiwalenga Wamarekani, hasa viongozi wa serikali.

Hatua ya Bessent kuhama imekuja baada ya jarida maarufu la Wall Street Journal kuchapisha makala inayoelezea na kuweka picha za makazi yake.

Makala hayo yalivipa wasiwasi vyombo vya usalama vya Marekani, vikiamini Iran inaweza kuwa imeshapajua anakoishi kigogo huyo.

Katibu huyo anaishi Georgetown, eneo ndani ya Washington, ambako ndiko makazi ya viongozi wengi wa Serikali ya Marekani na watu maarufu.

Related articles

Recent articles