LONDON, Uingereza
LEJENDARI wa Arsenal, Paul Merson, ameipa angalizo Chelsea akisema kushindwa kufuzu msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya litakuwa pigo kubwa kwa klabu hiyo.
Merson ameibuka na ujumbe huo baada ya kufuatilia mwendo wa kusuasua wa Chelsea, akieleza kutovutiwa na kiwango chao katika mchezo dhidi ya Sunderland wikiendi iliyopita.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 58, amesema kilikuwa ni kiwango kibovu zaidi cha Chelsea tangu msimu huu uanze.
Blues wakiwa ugenini, waliondoka vichwa chini baada ya kufungwa bao 1-0 na Sunderland, mfungaji akiwa ni Enzo Le Fee.
“Nilisikitishwa mno na kiwango chao dhidi ya Sunderland. Hawakucheza katika kiwango tulichotarajia kutoka kwao,” amesema.
Chelsea haipo Ligi ya Mabingwa baada ya kumaliza nje ya ‘Tano Bora’ ya Ligi Kuu ya England msimu uliopita.


