UYO, Nigeria
KIKOSI cha Taifa Stars kimewasili mjini Uyo, Nigeria, tayari kwa mchezo wake wa kufuzu fainali za AFCON 2027 dhidi ya wenyeji wao, Super Eagles.
Kwa mujibu wa taarifa, wachezaji walitarajiwa kuanza mazoezi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabio.
Stars itaikabili Nigeria Ijumaa ya wiki hii, licha ya kwamba timu hiyo imeshajihakikishia kushiriki kwa kigezo cha uenyeji ikishirikana na Kenya na Uganda.
Wachezaji na viongozi wa Stars wamewasili asubuhi ya leo Novemba 10, 2026, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Victor Attah.
Baada ya kutua na kumalizana na taratibu zote za Uwanja wa Ndege, msafara huo chini ya kocha Miguel Gamondi ulielekea moja kwa moja kwenye hoteli.


