16.1 C
New York

Ukraine, Urusi zamaliza kikao cha pili bila mwafaka

Published:

ABU DHABI, UAE

UKRAINE na Urusi bado ngoma mbichi. Mazungumzo ya kumaliza vita yaliyofanyika kwa siku mbili mjini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu [UAE], yamemalizika bila kupatikana kwa mwafaka.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na wawakilishi wa pande zote mbili, Urusi na Ukraine, huku Marekani ikiwa katikati kama msuluhishi.

Licha ya kutofikiwa kwa mwafaka wa moja kwa moja, Marekani imeeleza kuwa mazungumzo hayo yametoa picha nzuri kwa mustakabali wa vita hivyo vilivyodumu tangu mwaka 2023.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Ukraine, Davyd Arakhamia, amesema mazungumzo ya safari hii, ambayo ni ya kwanza tangu Februari, 2026, yamekuwa magumu zaidi.

“Naamini Urusi walikuja na maelekezo, hivyo ilikuwa ngumu kurahisisha mazungumzo,” amesema na kusisitiza kuwa anataka kuona pande mbili hizo zikirudi kwenye meza ya mazungumzo.

Baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, wajumbe wa Marekani, Steve Witkoff na mkwe wa Rais Donald Trump, Jared Kushner, wanatarajiwa kwenda Moscow, Urusi, kukutana na Rais Vladimir Putin, kisha kuelekea Ukraine kukutana na Volodymyr Zelensky.

Related articles

Recent articles