MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United iko mbioni kukamilisha dili la kumpa kazi kocha wa sasa wa timu ya soka ya Taifa ya Marekani, Mauricio Pochettino.
Pochettino anatajwa kuwa mstari wa mbele katika orodha ndefu ya makocha wanaohusishwa na kibarua cha kuinoa Man United.
Man United haijafikia uamuzi wa kumfuta kazi Michael Carrick lakini zipo taarifa kuwa ataondoka hivi karibuni.
Kwa sasa, ripoti zinaeleza kuwa mabosi wa Man United wako tayari kulipa Pauni milioni 7 kuvunja mkataba alionao Pochettino na Shirikisho la Soka la Marekani.
Endapo ataajiriwa, Muargentina huyo anaikuta Man United ikiwa hoi katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England msimu huu wa 2026-27.
Kwa sasa, kuna mapumziko ya kalenda ya FIFA, kisha Man United itarejea kwa mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Liverpool.


