14.4 C
New York

Nani kuvunja rekodi hii ya Ronaldo?

Published:

LONDON, Uingereza

CRISTIANO Ronaldo ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya Taifa ya Ureno akiwa amecheza mechi 234 na kufunga mabao 146 kwa miaka 23 aliyokuwapo kikosini.

Kwa idadi hiyo, ndiye mchezaji anayeongoza kwa kuzifumania nyavu akiwa na na timu ya taifa, akimzidi mabao 20 mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi.

Je, kwa kuwa Messi naye ameshastaafu kuitumia Argentina, nani anaweza kufikia idadi hiyo ya mabao ya Ronaldo?

ROMELU LUKAKU

Straika huyo ameshaifungia Ubelgiji jumla ya mabao 94. Kwa umri wake wa sasa, miaka 33, anahitaji mabao mengine 52 ili kumfikia Ronaldo. Je, ataweza?

HARRY KANE

Mshambuliaji huyo wa Bayern Munich ameshafunga mabao 91 katika mechi 125 za England. Kwa mwaka huu pekee, ameshaipachikia mara 13. Kwamba anahitaji mabao 55 ili kuifikia rekodi ya ‘CR7’.

KYLIAN MBAPPE

Amekuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia kwa misimu miwili mfululizo [2022 na 2026] na ndiyo kwanza ana umri wa miaka 27. Ameshafunga mabao 67 katika mechi 107 akiwa na kikosi cha Ufaransa.

ERLING HAALAND

Nyota huyo wa Manchester City ameshaifungia Norway jumla ya mabao 65 katika mechi 59. Alifunga matano katika mechi saba za Kombe la Dunia lililopita [2026]. Kwa umri wake, miaka 26, lolote linaweza kutokea.

LAMINE YAMAL

Ana safari ndefu kwani ndiyo kwanza ana mabao 11 akiwa na Hispania. Lakini, kwa kiwango bora alichonacho, pamoja na umri wake mdogo wa miaka 19, bado Yamal ana nafasi kubwa ya kufikisha mabao 146 ya Ronaldo.

Related articles

Recent articles